Bill Goats na Msitu

$ 14,90

Title: Bill Goats na Msitu
Author: Frode Burdal Klevstul
Translator: Flavian Mkupasi
Publisher: Curious Creators
Edition: First edition, 2022
Cover: Softcover
Pages: 52
ISBN: 978-82-692819-3-4

Ships From: US

This is a Print On Demand (POD) book. When we get a book order, the book will be printed within 5 business days. Then, the order will be packed and shipped from the US. Depending on your location, and how efficient the customs are where you live, it normally takes from 7 to 30 days from order to delivery is complete.

Out of stock

SKU: LHGB-46466816 Category: Tag:

Description

Palikuwa na msitu mmoja uliolifunika bonde moja ambalo lilijieneza tangu milimani mpaka baharini.

Msitu huo ulikuwa sehemu ya pekee, ukielezewa na wale walioujua kama mtulivu na salama; pia ulielezewa kama msitu wa kuvutia na wa hekima na wale walioujua vema zaidi. Lakini maneno hayakutosha kuuelezea, kwa kuwa njia pekee ya kuujua Msitu huo ilikuwa ni kuuishi.

Palikuwa na msemo mmoja wa kale, kwamba siku moja ndani ya Msitu huo ingeutakasa ubongo wenye mfadhaniko, wiki moja ingeupa afueni mwili wenye maumivu, mwezi mmoja ungeuondoshea moyo huzuni yake, na mwaka mmoja ungeiponya nafsi dhidi ya mizigo yake. Hivyo ndivyo Msitu huo ulivyotenda.

Yote yalikuwa makamilifu. Yote yalikuwa katika Usawa.

Halafu akaja Bill Goats pamoja na wafuasi wake mbuzi wa milimani. Bill Goats hakuuheshimu Usawa. Alitaka kuyadhibiti maisha.